Intra hukulinda dhidi ya ughushi wa DNS, aina ya shambulizi la mtandaoni linalotumiwa kuzuia ufikiaji wa tovuti za habari, mitandao ya kijamii na programu za kutuma ujumbe.
01
Uwazi zaidi katika ufikiaji wa intaneti
Intra hukuwezesha kufikia tovuti na programu zilizozuiwa kutokana na ughushi wa DNS, mojawapo ya mbinu zinazotumika zaidi kuweka vizuizi mtandaoni.
02
Ulinzi dhidi ya mashambulizi dijitali
Intra husaidia kukulinda dhidi ya wizi wa data binafsi na programu hasidi. Mashambulizi haya hutumiwa kuiba taarifa binafsi kama vile majina ya watumiaji na manenosiri au kuweka programu kwenye kifaa chako kwa kukuelekeza kwenye tovuti bandia.
03
Ulinzi bila kikomo kwa hatua moja tu
Intra ni rahisi sana kutumia — unaweza kuiwasha tu kisha uendelee na shughuli zako. Intra haitapunguza kasi ya muunganisho wako wa intaneti na hakuna kikomo cha matumizi ya data.
04
Teknolojia ya kuaminika
Intra hulinda faragha ya taarifa zako. Hatufuatilii programu unazotumia wala tovuti unazotembelea.
Intra hukuruhusu kuwekea mapendeleo huduma yako ya seva ya DNS. Unaweza kutumia seva yako mwenyewe au kuchagua miongoni mwa watoa huduma maarufu kama vile Cloudflare au Google.
Jinsi inavyofanya kazi
Intra husimba kwa njia fiche muunganisho wako wa intaneti kwenye seva ya umma ya Mfumo wa Majina ya Vikoa (DNS). Seva za DNS hufanya kazi kama orodha ya anwani — unapotumia intaneti, seva yako ya DNS hukupa anwani halisi unazohitaji kutembelea tovuti au kufungua programu.
Hata hivyo, seva za DNS zinaweza kubadilishwa ili kuzuia ufikiaji au kukuelekeza kwenye tovuti bandia. Kwa kusimba kwa njia fiche muunganisho wako kwenye seva za DNS katika kifaa chako cha Android, Intra husaidia kuhakikisha kwamba matokeo hayawezi kufanyiwa ughushi, kwa hivyo unaweza kufikia intaneti kwa njia salama.